PAGES

VIVUTIO VYA UTALII WILAYA YA GAIRO

VIVUTIO VYA UTALII VILIVYOPO WILAYANI GAIRO

Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ni miongoni mwa Halmashauri tisa (09) za Mkoa wa Morogoro. Ipo umbali wa Kilomete 133 kutoka Morogoro Mjini, upande wa Magharibu  mwa Mkoa, ikipitiwa na barabara kuu inayounganisha Mkoa wa Morogoro na Dodoma, pamoja na mikoa mingine ya Kanda ya Kati na Ziwa. Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ni miongoni mwa Halmashauri tisa (09) za Mkoa wa Morogoro. Sekta ya Utalii inakua kwa kasi kubwa katika wilaya hii, Sababu kubwa ya ukuaji kwa kasi ni  miundombinu inayojitosheleza inayofanya shughuli za utalii kufanyika kwa ubora wa hali ya juu. Miundombinu iliyopo ni pamoja na barabara kuu ya lami itokayo Morogoro kuelekea Dodoma ambapo ndipo makao makuu ya nchi yalipo. Zipo pia barabara za changarawe zinazounganisha vijiji, kata na Wilaya za jirani za Kongwa, Kilindi, Kiteto, Kilosa na Mvomero. Barabara hizi hupitika katika kipindi chote cha mwaka ingawa zipo barabara chache ambazo msimu wa mvua zinapitika kwa tabu kidogo kutokana na utelezi na mito kujaa maji. Aidha, ipo miundo mbinu ya umeme na simu katika maeneo mengi ya mjini na vijijini.

                                  Ndege adimu aitwae Moreaus sunbirds (Chisonyela)



Milima ya Ukaguru inayounda Safu za Milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountain) Jiografia ya Gairo imegawanyika katika uwanda wa tambarare na uwanda wa juu (milimani) ambao umetawaliwa na safu za milima ya Ukaguru ambayo ni sehemu ya safu za milima ya Tao la Mashariki (Eastern Arc Mountains). Sehemu kubwa ya milima hii ni Hifadhi za Misitu ya Taifa (Hifadhi za Taifa za Mamiwa kaskazini na Ikwamba pamoja na shamba la miti la serikali Ukaguru). Misitu hii ina ndege wa zaidi ya aina 60 wakiwemo ndege adimu duniani ambao ni; Rubeho Warbler (Endemic spp.), Moreaus sunbirds, Lubeck warbbel, Lubeck akalat, African tailorbird na Olive flanked robin pamoja na wanyama wadogowadogo kama vile Nyani, Kima, Komba, Ngedere, Tumbili, Galago (Bush baby), Panya, Vyura filimbi (Anthroleptis nikeae), vinyonga wenye pembe tatu, vipepeo na mmea adimu aina ya Lobelia sancta (Endemic spp), Macaranga capensis, Impatiens ukaguruensisi (Endemic) na Streptocarpus Schlieberii. Aidha, zipo hifadhi za misitu ya vijiji kwenye uwanda wa tambarare ikwemo hifadhi maarufu ya miti hadimu ya Mipingo ijulikanayo kama Leshata Vipigo Forest Reserve) uliopo katika kijiji cha Leshata.

Wanyama Adimu waliopo Ukaguluni. Maeneo ya ukagulu yana wanyama wengi ambao ni adimu kupatikana kwenye maeneo mengine, hivyo unapotembelea maeneo ya Ukagulu utanufaika kuwaona hao wanyama.

                                 Mnyama adimu anayepatikana Ukagulu


Maporomoko ya maji na Mapango ya Ukagulu. Katika Shamba la Miti Ukaguru yapo maporomoko ya maji yenye urefu wa mita 27 yajulikanayo kama “Ukaguru Waterfall” na Pango lenye sehemu nne (4) lililopo jirani na maporomoko haya. Wajerumani walikuwa wakijificha katika Pango hili ili kujihami dhidi ya maadui. Watalii wengi hutembelea eneo hili ili kuona na kufurahia madhari iliyopo. 

               KARIBU UFANYE UTALII WA NDANI WILAYA YA GAIRO








No comments:

Post a Comment

UTALII UKAGULUNI UMESHAFUNGULIWA TWENDENI TUKATALII WILAYA YA KILOSA NA GAIRO MKOANI MOROGORO.

 PICHA KATIKA MATUKIO YA UTALII UKAGULUNI. Wilaya ya Kilosa na Gairo zilizopo Mkoani Morogoro zimebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana ambavy...