LIFAHAMU
KABILA LA WAKAGULU
Karibu
katika Blog hii inayoeleza juu ya Kabila la Wakagulu ikiwa ni pamoja na
kufahamu historia yao kuhusu wapi walitokea na walifikaje katika Mkoa wa
Morogoro hasa katika Wilaya ya Kilosa na Gairo. Utajifunza mambo mengi
yawahusuyo Wakagulu ikiwa ni pamoja na Mila, Desturi na Tamaduni zao pamoja
na jinsi Koo zao zilivyotokea na zina
umuhimu gani katika maisha yao. Aidha, katika Blog hii lugha tatu zitatumika
ambazo ni Kikagulu, Kiswahili na Kingereza. Ungana nami kuyafahamu hayo yote.
Wakagulu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa na Gairo. Lugha yao ni Kikagulu. Wakagulu ni mojawapo ya makabila makubwa Mkoani Morogoro, Aidha wanapatikana pia katika Wilaya Kongwa, Kiteto na Mpwapwa Kiteto Mkoani Dodoma na sasa. wanatanuka zaidi maeneo ya Handeni na Mvomero Mkoani Tanga.
KARIBU
UJIFUNZE LUGHA YA KIKAGULU
No comments:
Post a Comment