PAGES

Monday, May 8, 2023

UTALII UKAGULUNI UMESHAFUNGULIWA TWENDENI TUKATALII WILAYA YA KILOSA NA GAIRO MKOANI MOROGORO.

 PICHA KATIKA MATUKIO YA UTALII UKAGULUNI.

Wilaya ya Kilosa na Gairo zilizopo Mkoani Morogoro zimebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana ambavyo kila mtu angependa kuviona, nakukaribisha kuona matukio katika picha yatakayokuonesha vivutio vya kitalii vilivyopo katika wilaya hizi. Karibu sana. 

KATI YA MAMBO UTAKAYOYAONA:-

1. Utalii kwenye Shamba la Ukagulu Gairo Mandege,

2. Mafufumo Waterfalls

3. Vipepeo wazuri na Vinyonga wenye mapembe

4. Mandhari nzuri ya Kubalizi Milima ya Rubeho Mamiwa na Nongwe.

5. Wanyama wazuri Pamoja na Bush baby wa kitofauti.


















YOHANA MSUNHILE

MKUTANO MKUU WA WAKAGULU WA MWAKA 2022










Monday, April 12, 2021

UKOO WA WANJEJA

WANJEJA

Kama historia inavyoonesha jinsi wakagulu walivyosafiri kutoka maeneo ya Rwanda na Burundi wakitokea Afrika ya kusini na kisha kuingia Tanzania kupitia na kuweka vituo  vya mapumziko kwa muda maeneo KONONGO (UKIMBU), Mkoani Rukwa baadaye walipita maeneo ya Mkoa wa Singida hadi wakaingia RUDI (KUSINI MWA MPWAPWA). Wanjeja ni kati ya koo za Kikagulu ambazo zilipatikana baada ya kutoka Kondoa Irangi Mkoa wa Singida na kufika maeneo ya Mlima ng’hili uliopo Kitange wakiwa bado hawana koo, kilichotokea ni kwamba kila tukio lililotokea wakiwa safarini lilisababisha wenzao wawaite jina la hilo tukio au sehemu waliyopumzika au kulala na kisha watu hao kuonekana kuwa ndio ukoo wao. Katika mlima Ng’hili kati ya Milima ya Itumba au Mamboya kulikuwa na miti inayoitwa Minjeja, hata sasa inapatikana katika maeneo ya Kitange, Sasa mmoja kati ya hao Wakagulu alifika kwenye Mlima huo na akalala chini ya mti wa Mnjeja hivyo basi asubuhi walipoamka wenzake wakamwita mnjeja ng’hili. Bibi mwingine ambae alikuwa mmoja kati ya waliolala kwenye mti mnjeja alikuwa anaitwa Haba (Mdala Haba).

Wakiwa katika eneo lao la Ng’ili walisikia kuwa kwenye eneo la Wasindugu ukoo mwingine ambao walikuwa eneo la tambalale kulikuwa na shida ya watu kuuwawa na mnyama mkali (Ikala) Kwa wakagulu wanapotumia neno “Ikala” humaanisha mnyama mkali kama vile Simba au Chui ambao ni hatarishi kwa maisha ya binadamu. Baada ya kusikia hivyo wanaukoo Wanjeja wakawaambia Wasindugu kuwa tuna bibi yetu Haba atawasaidia, Bibi haba alienda huko kwa Wasindugu na alipofika akawaambia wamjengee kanyumba kadogo kawe mtego kwa kikagulu wanaita Ilundi. Nyumba hiyo ina vyumba viwili, chumba cha mbele wakamuweka bibi huyo wakafunga mlango, chumba cha pili kilikuwa mwanzoni kabisa wakaweka bunduki mlangoni ambayo waliitegesha kuelekea mlangoni wakati huo wametegesha pale mlangoni kama kitu kitakanyaga kamba itafyatua bunduki. Huyo mnyama mkali alipofika mlangoni alikanyaga ile kamba na kuifanya bunduki kufyatuka na kumuua.

Baada ya risasi kufyatuka na yule bibi kusikia mshindo wa mnyama akianguka, alipiga vigelegele, ndipo Wasindugu wakaja na kumwambia atoke nje wajadiliane na kumshukuru kwani tayari mnyama mkali ameshakufa. Bibi Haba akasema mimi sitoki nje, wakamwambia basi tutakupa Mbuzi au ng’ombe, yule bibi akaendelea kukataa. Kwa kipidni hicho hakukuwepo fedha kama njia ya kufanya manunuzi au kumpa mtu kama ujira, mwishoni yule Bibi akasema nipeni eneo la kumiliki kwenye hili eneo lenu mlilonalo ili eneo hilo liwe langu. Wasindugu wakakubali kumpa eneo ambalo kwa sasa linajulikana kwa jina la Njoge.

Kwenye eneo hilo kulikuwa na pango kubwa ambalo lilikuwa linatoa maji, ambako Wasindugu walikuwa wanachota maji, hadi sasa sehemu hiyo ndiko watu wa eneo hilo wanachota maji.

Siku moja bibi huyo alikwenda kuchota maji, kwa bahati mbaya lile pango likabomoka na kufunga sehemu ya kuingilia hivyo akakwama kwenye tope hilo na ndio ukawa mwisho wa maisha yake. Kuanzia siku hiyo watoto waliokuwa wakizaliwa kwenye ukoo huu wanaume wanaitwa MKWAMA ikimaanisha kuwa bibi alikwama kwenye tope na wanawake wanaitwa MANJOGE maana yake walipokuwa wanafukua udogo ulioporomoka kumtoa yule bibi walikuwa wanakuta wadudu ambao huwa wanapatikana katika mabwawa ya maji wanaoitwa Njogela. Hadi leo eneo hilo linaitwa njoge lipo maeneo ya Pandambili.

Kwahiyo wanjeja wamegawanyika makundi mawili yaani Wanjeja Ng’ili na Wanjeja Njoge

Msimulizi Elias Yohana Mwendi (Mlegu)


Mwandishi Cuthbert Yohana Mwendi (Mkwama)


HISTORIA YA WAKAGULU


HISTORIA, MILA NA DESTURI ZA WAKAGULU

Wakagulu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikagulu. Wakagulu ni mojawapo ya makabila makubwa katika mkoa wa Morogoro, Wakagulu zaidi wapo katika Wilaya za Kilosa, Gairo, Mpwapwa, Kongwa, Kiteto na sasa wanatanuka zaidi maeneo ya handeni. Ukifuatilia Simulizi za wazee, hususani wakati wa sherehe za kumaliza msiba (mwidiki) inaonesha kuwa Wakagulu walitokea maeneo ya Rwanda na Burundi (yasasa). Walitoka maeneo hayo kutokana na ukame uliokuwepo na matatizo mengine ya kivita. Walipita maeneo mengi yakiwemo KONONGO (UKIMBU) Mkoani Rukwa baadaye walipita maeneo ya Mkoa wa Singida hadi wakaingia RUDI (KUSINI MWA MPWAPWA). Baada ya kuishi hapo kwa muda waliparamia milima ya Lubeho, lakini bado walikuwa na mawasiliano makubwa na watu wa Konongo. Katika kuzunguuka hapa na pale huko milimani ndipo zilipojitokeza Koo mbalimbali za wakagulu kutokana na matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiwapata wanawake. Kwa msingi huo Wakagulu wanachukua ukoo kutoka kwa mama (Welekwa). Kwa mfano ukoo wa Wambigo ulipatikana baada ya wahenga kukanyaga maji yaliyokuwa yanajizunguusha (Gakubiga) kwenye mto Mkondoa  na Ukoo wa Wanjeja wao walipata jina la ukoo wao baada ya kufanya safari ndefu na ulipofika usiku walienda kulala kwenye mti unaoitwa MNJEJA. Hao ndio Wakagulu. 





Monday, October 9, 2017

UTALII UKAGULUNI UMESHAFUNGULIWA TWENDENI TUKATALII WILAYA YA KILOSA NA GAIRO MKOANI MOROGORO.

 PICHA KATIKA MATUKIO YA UTALII UKAGULUNI. Wilaya ya Kilosa na Gairo zilizopo Mkoani Morogoro zimebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana ambavy...