Monday, April 12, 2021
UKOO WA WANJEJA
Baada ya risasi kufyatuka na yule bibi kusikia mshindo wa mnyama akianguka, alipiga vigelegele, ndipo Wasindugu wakaja na kumwambia atoke nje wajadiliane na kumshukuru kwani tayari mnyama mkali ameshakufa. Bibi Haba akasema mimi sitoki nje, wakamwambia basi tutakupa Mbuzi au ng’ombe, yule bibi akaendelea kukataa. Kwa kipidni hicho hakukuwepo fedha kama njia ya kufanya manunuzi au kumpa mtu kama ujira, mwishoni yule Bibi akasema nipeni eneo la kumiliki kwenye hili eneo lenu mlilonalo ili eneo hilo liwe langu. Wasindugu wakakubali kumpa eneo ambalo kwa sasa linajulikana kwa jina la Njoge.
Kwenye eneo hilo kulikuwa na pango kubwa ambalo lilikuwa linatoa maji, ambako Wasindugu walikuwa wanachota maji, hadi sasa sehemu hiyo ndiko watu wa eneo hilo wanachota maji.
Siku moja bibi huyo alikwenda kuchota maji, kwa bahati mbaya lile pango likabomoka na kufunga sehemu ya kuingilia hivyo akakwama kwenye tope hilo na ndio ukawa mwisho wa maisha yake. Kuanzia siku hiyo watoto waliokuwa wakizaliwa kwenye ukoo huu wanaume wanaitwa MKWAMA ikimaanisha kuwa bibi alikwama kwenye tope na wanawake wanaitwa MANJOGE maana yake walipokuwa wanafukua udogo ulioporomoka kumtoa yule bibi walikuwa wanakuta wadudu ambao huwa wanapatikana katika mabwawa ya maji wanaoitwa Njogela. Hadi leo eneo hilo linaitwa njoge lipo maeneo ya Pandambili.
Kwahiyo wanjeja wamegawanyika makundi mawili yaani Wanjeja Ng’ili na Wanjeja Njoge
HISTORIA YA WAKAGULU
HISTORIA, MILA NA DESTURI ZA WAKAGULU
Wakagulu ni kabila la Tanzania wanaoishi katika Mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Kilosa. Lugha yao ni Kikagulu. Wakagulu ni mojawapo ya makabila makubwa katika mkoa wa Morogoro, Wakagulu zaidi wapo katika Wilaya za Kilosa, Gairo, Mpwapwa, Kongwa, Kiteto na sasa wanatanuka zaidi maeneo ya handeni. Ukifuatilia Simulizi za wazee, hususani wakati wa sherehe za kumaliza msiba (mwidiki) inaonesha kuwa Wakagulu walitokea maeneo ya Rwanda na Burundi (yasasa). Walitoka maeneo hayo kutokana na ukame uliokuwepo na matatizo mengine ya kivita. Walipita maeneo mengi yakiwemo KONONGO (UKIMBU) Mkoani Rukwa baadaye walipita maeneo ya Mkoa wa Singida hadi wakaingia RUDI (KUSINI MWA MPWAPWA). Baada ya kuishi hapo kwa muda waliparamia milima ya Lubeho, lakini bado walikuwa na mawasiliano makubwa na watu wa Konongo. Katika kuzunguuka hapa na pale huko milimani ndipo zilipojitokeza Koo mbalimbali za wakagulu kutokana na matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiwapata wanawake. Kwa msingi huo Wakagulu wanachukua ukoo kutoka kwa mama (Welekwa). Kwa mfano ukoo wa Wambigo ulipatikana baada ya wahenga kukanyaga maji yaliyokuwa yanajizunguusha (Gakubiga) kwenye mto Mkondoa na Ukoo wa Wanjeja wao walipata jina la ukoo wao baada ya kufanya safari ndefu na ulipofika usiku walienda kulala kwenye mti unaoitwa MNJEJA. Hao ndio Wakagulu.
Subscribe to:
Posts (Atom)
UTALII UKAGULUNI UMESHAFUNGULIWA TWENDENI TUKATALII WILAYA YA KILOSA NA GAIRO MKOANI MOROGORO.
PICHA KATIKA MATUKIO YA UTALII UKAGULUNI. Wilaya ya Kilosa na Gairo zilizopo Mkoani Morogoro zimebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana ambavy...

-
PICHA KATIKA MATUKIO YA UTALII UKAGULUNI. Wilaya ya Kilosa na Gairo zilizopo Mkoani Morogoro zimebarikiwa kuwa na vivutio vingi sana ambavy...